Shambulizi la kushitukiza lililotokea katika mkoa wa magharibi Sudan Darfur umesababisha vifo kwa wanajeshi 7 watanzania pia kusababisha majeruhi kwa wengine kumi na saba.
Naibu waziri wa wizara ya mambo ya nje ya nchi Mahadhi Juma Maalim alioneshwa kusikitishwa na shambulio hilo lililochukua uhai wa wanajeshi wa Tanzania.
'
'Tanzania tumesikitishwa sana na mashambuizi haya ambayo yamesababisha mauaji ya sakari wetu ambao walikwenda huko kulinda amani\.alisema Malim
Chanzo kinasemekana ni kuzungukwa kwa ghafla kwa wanajeshi wa Tanzania baada ya mtego wa kumkamata mwenzao amabapo kikundi hicho kilijua atafuatwa kuokolewa ili watimize shambulizi lao.
Pia katika shambulizi hilo kikundi kilichoshambulia kilikuwa na silaha za nguvu huku mojawapo ikiwa ni rocket drivs grenedas chenye uwezo wa kushambuli umbali wa km 25[15 maili}.
Darfur kumekuwa na mauaji yazaidi ya watu 3000,000 Tangu mwaka 2003.Toka mwaka 2009 rais wa Sudani Omar al Bashir anasakwa na mahakama ya mauaji ya kimbari kutokana na vifo hivi vilizyosababisha Suadna kugawanyika.
Kwa miezi mitano tu ndani ya mwaka huu watu 300,000 wamekimbia mapigano nchini humo.
Nch arobaini zimechangia wanjeshi kuilinda Darfur huku ikiwa na jumla ya wanjeshi 16,500 na polisi zaidi ya 5000 wa kimataifa.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani shambulizi hilo.
MAJINA YA WALIOKUFA YAPO CHINI
Hawa ndio askari waliopoteza maisha huko Sudan walikuwa katika vikosi vya Umoja wa Mataifa vya
kulinda amani Sudan.
1.Pte Rodney Ndunguru
2.Pte.Peter Werema
3.Pte.Fortnatus Msofe
4.Koplo Mohammedi Chilikizo.
4.Sajenti Shaibu Athumani
5.Koplo Oswald Chaula
6.Koplo Mohameddi Juma





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni