Jumatatu, 15 Julai 2013

MANCHESTER UNITED YATANGAZA OFA KWA FABREGAS.......

Klabu ya Manchester united imeamua kujaribu harakati nyingine katika harakati za kuboresha kikosi chake msimu ujao safari hii imemgeukia Cecs Fabregas baada ya kumkosa Thiago Alcantara.

Klabu ya Manchester United ilikuwa inahitaji huduma za Thiagho Alcantara kwa kuziba pengo la mchezaji aliyetundika daruga Paul Schooles.

Fabregas kwa sasa hana nafasi kubwa katika klabu yake ya Barcelona  na kwa vyovyote atahitaji kupata nafasi nyingine ili aweze kucheza zaidi ingawa hajawahi kuthibitisha kuikacha miamba hiyo ya Catalunya.

Ofa ya paun milioni 25 imewekwa na klabu ya Manchester unite inaweza kuamua kitu siku chache zijazo ambapo inasubiri klabu ya Barcelona itaamua nini juu ya ofa hii.

Pia Arsenal wamehusishwa sana kutaka kumrejesha tena mchezaji wake wa zamani huyu katika kipindi hiki amabacho klabu yake inataka kujihimarisha .



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni