Jumapili, 7 Julai 2013

NDEGE YAGONGA UKUTA WA BAHARI NA KUUA WATU 2 NA KUJERUHI 181

Ndege aina ya Boeng 777 imeua watu wawili huko San Francisco nchini Marekani baada ya kugonga ukuta wa Bahari na kulipuka huku ikiacha majeruhi 181


.

Ndege hii ambayo ilikuwa ianonekana kushuka haraka sana huku ikiwa ipo salama laikini iligonga ukuta wa bahari na kuvunjika mkia na kuanza kupoteza mweleko pamoja na kunyofoka kwa injini.

Mkuu wa kampuni hiyo ya Korea Kusini Asian Yoong Youn Doo alisema kuwa sababu ni za kiufundi au mitambo ni matatizo ya kiabinadamu.

Alisema marubani pia walikuwa ni wazoefu na maveterani wa usafirishaji wa anga na aliomba radhi kwa wote waliothiriwa na ajali hiyo kwa ndege ambayo ilikuwa ni salama sana kwa siku nyingi.

Ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria 261 wafanyakazi 16 .Kulikuwa na wachina 141,wakorea kusini 77 na Wamerekani 61.Mpaka sasa watu wawili wameripotiwa kufariki wote wachina na abairia 181 wapo hospitali kwa matibabu.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni