Vannesa Kimei mama Mzazi wa marehemu Langa kileo maarufu kama Langa amefunguka kuwa kama angekuwepo Tanzania Langa asingepoteza maisha.Alisema wakati amabao mwanaye anaanza kuumwa,Yeye alikuwa nchini Marekani ambako alienda kumuona mwanaye mwingine aliyekuwa ameifungua.
“Wakati mwanangu ameanza kuumwa sikuwepo, nilikuwa safarini Marekani nilikoenda kumuona mwanangu wa kike aliyekuwa amejifungua, kwa mila za kwetu ni lazima mama kwenda kumuogesha mtoto lakini ningekuwepo mwanangu asingeondoka jamani,’’ alisema mama Langa.
mama na baba wa marehemu Langa Kileo
Mama Langa alisema kuwa Langa kila anapoumwa yeye huwa anamtibu mwenyewe katika vipindi mbalimbali ambayo anaumwa kuna wakti anamwekea hata dripu pale anapozidiwa.Kama asingeenda Marekani angebaki na mwanaye Langa asingefariki yeye anaamini kwani ni mara nyingi umtibu mwanaye
“Nilikuwa namuwekea dripu za dawa mwanangu hapahapa nyumbani, alikuwa anaugua kwa muda na kisha anarudi katika hali ya kawaida,” alisema kwa uchungu mama Langa.
Hata hivyo baadhi ya waombolezaji waliokuwepo msibani walimsihi mama huyo kukubaliana na mipango ya Mungu kwamba kila mwanadamu lazima atakufa, hali iliyompa faraja na kumfanya anyamaze.
Marehemu Langa aliyefariki baada ya kusumbuliwa na kile kilichoelezwa kuwa ni ugonjwa wa malaria kali na homa ya uti wa mgongo, alizikwa Jumatatu iliyopita katika Makaburi ya Kinondoni, Dar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni