Huku vyombo vya habari vikizidi kuripoti habari juu ya mshambuliaji hatari wa Manchester United Wayne Mark Rooney kuwa atajiunga na klabu fulani,Meneja mpya wa Real Madrid naye kaingia kati katika vita hiyo.
Carlo Ancelotti amemtaja Rooney kama hitaji lake katika klabu yake mapya.Sasa inawezekana Christiano Ronaldo akabadilishana jezi na Rooney kwani Man U wanahitaji huduma yake.
Kauli ya Rais wa zamani wa Los Blanos Ramon Calderona kusisitiza Ronaldo auzwe kama hana furaha klabuni hapo inaweza kuchochea hasira kwake kutofurahi kakaa klabuni hapo.
Manchester united ipo katika mbio za kusaka saini y nyota wake huyo wa zamani kipindi hiki na hasa kama Rooney atathibitisha kuondoka Mancheter.Ingawa Rooney hataki kuuzwa nje ya Uingerza huku Chelsea ikiwa chaguo lake la kwanza.Cha kushangaza Man U hawapo tayari kummuza kwa dau lolote Chelsea kwani ndio washindani wao wakuu msimu ujao

.jpg)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni