Jumamosi, 29 Juni 2013

MKE WA ZAMANI WA MANDELA AELEZA JAMBO JIPYA KUHUSU MANDELA

Mke wa Zamani wa Nelson Mandela Winnie Madikizela-Mandela amesema kuwa hali yake Mzee Madiba imeboreka kwa kiwango kikubwa kuliko siku chache zilizopita.
Akizungumza nyumbani kwake na waandishi wa habari alisema pamoja na kuwa na hali mbaya kwa kuwa anachoumwa ni kitu kikubwa lakini ni afadhali sana kuliko siku chache zilizopita.
Binti wa Mandela Makaziwe alisema
kuwa baba yake ingawa alikuwa na hali mbaya ila aliweza kuona na kugusa.
Mandela yupo katika hospitaliya Petroria Mediclinic kwa takribani siku ishirini.
WINNIE MANDELA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni