HAWA NDIO WAMEMPELEKA BARCELONA EMANUEL OKWI
Na hosea Mchopa
Maneno mazito husukuma moyo uende haraka hasa pale yanapokugusa na kuweka wazi ukweli.Wafalme siku zote ni waharibifu hutaka kuchagua kila kitu wahisicho wanapenda wao kukifanya.Wafalme hawa siku zote huwekwa na watu ambao baadaye hujilaumu milele na milele.
Kocha wa zamani wa Hispania Javier Clement alitumia mtandao wa twiiter kuchoma moto pori kwa maandishi ambayo yamegusa pale wengi wameshindwa kugusa.Kawa jasiri kuweka wazi ugomvi wa Barcelona kuwa umetengenezwa na wenyewe bila kujua na sasa wanaaonja tamu yake.
‘’Wanafanya mazoezi pale wanapotaka,wanacheza pale wanapopenda,wana sikukuu ndefu kuliko wengine,na wanachagua makocha wao,Siku zote naamini kundi ni muhimu kuliko mtu mmoja’’.Javier Clement kaonesha upande wa pili wa wanaomdhania ni mfalme kuwa anaishi nje ya weledi wa taaluma yake.
Nani kamleta mfalme Lionel Mess huku hadi haisi ule msemo maarufu wa klabu ya Brcelona ‘’more than a club’’.Uwe hauna nguvu mbele yake.Wakatulunya wa Barcelona wanaamini mchezaji muhimu kwao ni yule aliyewekea roho yake rehani kwa ajili ya klabu na ataakubali kuwa nyuma ya klabu daima.Si siri tena mambo ya Mji wa Dar es Salaam yanayofanywa na Mganda Emmanuel Okwi yamesafiri mpaka La Liga nani kayapeleka.
Mshambuliaji wa klabu ya Simba Emmanuel Okwi
Hivi karibuni iliripotiwa Mfalme wa Barcelona Lionel Messi kufanya mazoezi peke yake kwa jumla ya masaa 24.Ukiacha zile ripoti za kukacha kabisa mazoezi.Messi ambaye timu ya Barcelona ikiwa nyuma yake imemsaidia kuweza kutwaa tuzo za uchezaji bora wa mwaka duniani mara 4.Ameripotiwa kuzozana na kocha ambaye pia ni zao la klabu ya Barcelona na nchi ya Hispania Luis Enrique baada ya kichapo cha goli 1 -0 kutoka kwa Real Sociedad na yeye kuwekwa nje.
Jeuri ya Lionel Messi ni kubwa kwa sasa kutokana na adhabu ambayo klabu ya Barcelona inaitumika ya kutosajil dirisha hili na lijalo.Hali iliyopelekea mkurugenzi wa michezo Andon Zubizarreta kufukuzwa kazi.Lakini kutokana na weledi mkubwa alionao Enrique jeuri yake inaweza kuwa kubwa zaidi ya Messi kama akipewa muda kwani anaijua Barca vilivyo na wala hataaingaika zaidi ya kuwapa vijana wadogo nafasi.Tukumbuke Barcelona ina Allen Hillalovic,Traore ambao wanauwezo mkubwa sana kama wakipewa nafasi.Tusisahau Luis Suarez na Neymar pia ni mmoja ya wachezaji wanaoweza kumpa kiburi Enrique.
Josep Bartmoe rais wa klabu ya Barcelona ameshindwa kuweka wazi hali inayoendelea katika klabu yake kwa kuhofia itavuruga mambo.Tabia hii haina utofauti na ya viongozi wa klabu ya Simba wanavyomlealea Emanuel Okwi wakidhani wanamfurahisha kumbe wanamuharibu kwa kasi ya ajabu na hasara ya pesa ya kumsajili itakuja kuwaumiza siku atakapoamua kuchagua mechi za Simba na yanga kama sasa hivi anapoamua kulikacha kombe la Mapinduzi.
Kocha Enrique anaonekana hana mwanga mwembamba kuona hali iliyo ndani ya klabu yake.Bado anaamini maendeleo ya klabu yanamsisimua na yanampa matumaini makubwa kwa kuwa wachezaji wake wanafanya kila anachotaka.Kwa kauli hii kama Messi anahitaji kocha aamue kama yeye anavyohitaji hana utoafuti wowote na Emanuel Okwi.Swali ni nani kachangia kumfanya Messi awe hivi.
March 13 mtandao wa fitbathatba ulimnukuu Messi akisema Guardiola ni mtu muhimu katika klabu ya Barcelona.Guardiola alitengeneza timu kumzunguka Messi,alipewa kila mpira ulio hatari akazidi kumfanya Messi awe mfalme.Messi akaitawala dunia akatwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka duniani mara nne.Kocha gani hukosa presha pale aunapo uso wa Lionel Messi.Basi Guardiola akapunguza hadi ukali pale Messi alipopita mbele yake.
Tito Vilanova,Pep Guardiola na Tata Maratino wote walimtengeneza Messi kama mfalme wa klabu kama walivyomkuta.Kama walivyoona mashabiki wanamuheshimu Messi kuliko kitu chochote.Upekee wa huduma waliokuwa wanampa kuanzia ndani ya uwanja.Mfumo mzima wa kucheza kumzunguka yeye,kupewa mipira iliyokufa,pealti na mipira yote muhimu ndani ya eneo la hatari.Uongozi unavyomnyenyekea nje ya uwanja kuweza kupewa mapumziko kirahisi kulikoni mwingine yalimjenga Messi kuwa hivi.Ndio wakafanya taswira ya Messi istofautiane sana na Emmanuel Okwi.
Guardiola mpya Luis Enrique kama ilivyotambulishwa alipolamba dili la kuifundisha AS Roma kwa miaka miwili yeye hana hulka kama za Guardiola mwenyewe kumuabudu mchezaji yoyote.Enrique yeye ni kocha anayeishi kwa kufuata nidhamu kama msingi mkuu na kuamini katika timu wala si mchezaji mmoja.Yeye hana tofauti na Louis Van Gaal ambaye amemaliza ufalme wa Rooney baada ya Moyes kushindwa kuukomesha.Hana tofauti na Javier Clement pale anapopewa madaraka ya ukocha huamini yeye ni kiongozi wa kikosi kizima.
Alipotua Stadio Olimpico Roma alifanya maajbu makubwa sana ya kupamabana na wafalme waliotengenezwa miaka mingi katika klabu hiyo.Daniel De Rossi pamoja na Fransico Totti walipambana na roho ya udikteta wa nidhamu wa Enrique.Hakuweza kuvumilia kuona Danie De rossi anachelewa katika mechi ya maandalizi kwa sababu ni mkongwe wa timu.Hakuwa na mashaka kumwacha nje nahodha wa timu Totti baada ya kuvunja sheria zake za kutofanya mazoezi ipasavyo kabla ya mechi.
Ni ngumu sana tena haitowezakana kocha anayefata weledi kusihi na mfalme vizuri siku zote,unakumbuka David Bekham na Ferguson.Kupitia mtandao imeripotiwa Messi amemtaja kama Frank Rjakard ni kocha anayefaa kuchukua mikoba ya Enrique.Leo hii ufalme anaopewa Okwi Simba kocha yoyote anayeongozwa kwa misingi ya nidhamu hawezi kuishi nae vema.Chagua ni moja kuendelea kukumbatia bomu litakalolipuka baadaye au kufanya maamuzi magumu kumuuza mfalme.
Enrique akutengeneza hali ya upekee wowote kwa nahodha Totti alipokuwa Roma.Alihakikisha wote ni sawa.Hiki kitu Messi anakikosa sasa na anakumbuka zama za Guardiola na ujio wa Neymar na Luis Suarez unaweza ukapunguza mafanikio makubwa binafsi hasa pale wachezaji hawa watakapoiva na utamaduni wa Barcelona.
Lionel Messi wa vilanova alikuwa anafurahia kila kitu hasa uongozi wa timu na benchi la ufundi linavyompa nafasi ya upekee.Viongozi wa Barcelona kujisahau kwa Messi kunaweza kusababisha hata Hillalovic ambaye ni Messi mpya kuchelewa kuleta matunda.Enrique haoni shida kumweka Messi nje pale atakapoonekana kutaka ufalme mbele yake.Siku zake zaweza kuwa zinahesabika kwa sababu ya tabia za viongozi kuwatumia wafalme katika kupata kura kama afanyavyo sasa Josep Bartomeu.Ndivo Perez hufanya kwa Cristiano Ronaldo,Hivi hivi viongozi wa Simba humtumia Okwi katika kujipatia nafasi katika mioyo ya mashabiki.
Emmanuel Okwi
Kwa kiwango cha soka la Tanzania sikuwahi kufikiria kama tutakuja kumpenda mtu kiasi cha kumuharibu bila kujua hiliali kesho tutamlaumu.Siamini heshima na hamasa anayopata Emmanuel Okwi anajajihisi yupo afrika hii.Leo hii anahitaji hata kufanya kila anachotaka kulikoni kocha alichomtuma.Na anajua viongozi wanaomwabudu wapo na wala hatapata tabu yoyote.Hii inampa kiburi aweze kufunga ndoa hata kama timu ipo kambini.Anaweza kukukaa kwao na akarudi siku moja kabla ya mechi na akaingia uwanjani tena kikosi cha kwanza.
Kuna muda mashabiki wa Barcelona watahitaji kumsahau Messi alipoingia kwa mara ya kwanza oktoba 16 mwaka 2004 akiingia kuchukua nafasi ya Deco mgongoni akiwa na jezi namba 30 akiingia kupambana na Espanyola.Watahitaji kuona klabu ya Barcelona inapata heshima na hapo wataona makosa ya kumtengeneza Mfalme bila misingi.
Historia yake haitafutika Fabio capello alipata fadhaiko sana kwa mara ya kwanza alipokutana na huyu kijana katika El classic alipoamua kufunga hat trick yake ya kwanza katika la liga dhidi ya Real Madrid.Mzee Wenger aliwaza sana kuhusu akunti yake pasipo kujisikilizia sifa akizomwaga ingepasa awe ndani ya London.Huu ndio ulikuwa mwanzo wa kumtengeneza mfalme ambaye hatakuja kudhani timu ina historia kubwa kulikoni yeye.