Familia hii yenye wake watatu,watoto 6,wajukuu 17 na watukuu 12 ipo kwenye mgogoro mkubwa sana amabapo Mandla mjukuu wa Mandela anashutumiwa kufukua miili ya ndugu zake bila ya idhini kutoka katika familia.
Mandla ambaye inasemekana ni mmoja ya watu wanadhaniwa kufaa kuwa mrithi wa Mandela katika familia japo hakubaliwi na wengi kutokana na maamuzi yake.
Mandla ailfukuu mwili wa babayake aliyefariki 2005 kwa ukimwi,pia,ndugu zake na mwanawe.Kitu amabacho kimepingwa mahakamani na familia kuwa si sahihi kuamua peke yake.
Lakini Mandla Mandela, ambaye kulingana na vyombo vya habari, alihamisha maiti hao umbali wa kilomita 22 kutoka mji wa wa Qunu hadi nyumbani kwake eneo la Mvezo mnamo mwaka 2011, anapinga uamuzi huo.
Kufukua kwa maiti kunaonesha kuwa Familia hii ipo kwenye mgogoro mzito.Huku watoto wa kike wa Mandela Makaziwe na Yenani wakipinga kitendo hicho.
KWA IMANI ZA ASILI ZA AFRIKA KUSINI ZINASEMA HIVI
Mtu huwa hafi kama kuna kitu kinamsubiri kusuluhisha hasa kwa watu wenye hekima kama Mandela.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni